×

Iran Yatajwa Kwenye Hali ya Kuporomoka, Trump Aibua Sakata la Hormuz

Rais wa Marekani, Donald Trump.

Rais wa Marekani, Donald Trump, amedai kuwa Iran imewafahamisha Marekani kwamba ipo katika “state of collapse” na imeomba kufunguliwa kwa njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta ya Strait of Hormuz haraka iwezekanavyo.

Kwa mujibu wa kauli hiyo aliyoiweka kwenye mtandao wa Truth Social, Trump amesema Iran inajaribu kushughulikia changamoto za uongozi wake huku akidai anaamini nchi hiyo itaweza kujipanga upya.

Hata hivyo, taarifa hizo hazijathibitishwa rasmi na serikali ya Iran, jambo linaloacha maswali kuhusu ukweli wa madai hayo.

Strait of Hormuz ni njia muhimu sana ya baharini duniani, ambapo sehemu kubwa ya mafuta yanayosafirishwa kutoka Mashariki ya Kati hupita, hivyo kauli zinazohusiana na eneo hilo mara nyingi huibua mjadala mkubwa wa kimataifa na kiuchumi.

Leave a Comment