×

Waziri wa Madini Anthony Mavunde Azindua Tawi Jipya la Exim Geita

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ambaye alikuwa mgeni rasmi, amefanya uzinduzi wa tawi jipya la Exim Bank Tanzania katika Mkoa wa Geita kwa kukata utepe kuashiria kuanza rasmi kwa huduma za benki hiyo katika eneo hilo.

Katika hafla hiyo iliyofanyika Mei 9, 2026 mjini Geita, Waziri Mavunde alikuwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba, viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na viongozi wa benki hiyo.

Pia katika tukio hilo alikuwepo Afisa Mtendaji Mkuu wa Exim Bank Tanzania, Jaffari Matundu ambaye alieleza dhamira ya benki hiyo kuendelea kusogeza huduma za kifedha karibu zaidi na wananchi pamoja na kusaidia kukuza shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Geita na maeneo jirani.

Ufunguzi wa tawi hilo unatajwa kuwa hatua muhimu katika kuimarisha huduma za kifedha na kuongeza fursa za biashara kwa wakazi wa Geita, hususan katika sekta ya madini, biashara na uwekezaji.

Leave a Comment