×

Watu Wawili Wafariki, 12 Wajeruhiwa Ajali ya Basi Iringa – Video

Watu wawili wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa, wakiwemo raia wanane wa Zimbabwe na raia wanne wa Zambia, kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyohusisha basi kubwa la abiria la kampuni ya THE CLASSIC linalofanya safari zake kati ya Zimbabwe na Tanzania pamoja na lori la mizigo, baada ya magari hayo kugongana uso kwa uso katika Kijiji cha Uyole, Kata ya Mseke, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Baadhi ya abiria ambao wamenusurika ktk ajali hiyo kwenye anaeo la ajali wameelezea kile ambacho wamekiona huku wengi wakisema tukio hilo limewakuta wangali wakiwa usingizini.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dkt. Alfred Mwakalebela amethibitisha kutokea kwa vifo viwili na majeruhi 13 ambapo kati yao watu 8 ni raia wa Zimbabwe na wanne raia wa Zambia.

Leave a Comment