×

Yanga Yatozwa Milioni 30, Meneja Wake Afungiwa Michezo Mitatu

YANGA imetozwa faini ya Sh milioni 30 kwa kosa la wachezaji pamoja na maofisa wa benchi la ufundi kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo Stadium na badala yake kutumia nyumba iliyopo nje ya uwanja huo upande wa pili wa barabara.

Tukio hilo lilitokea Mei 3, 2026 wakati wa mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Kwa mujibu wa Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Tanzania Premier League Board (TPLB), kitendo hicho ni ukiukwaji wa Kanuni za Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo.

Mbali na adhabu hiyo, Yanga pia imepewa onyo kali baada ya kuchelewa kuwasili uwanjani kwa mchezo huo, ikifika saa 10:35 alasiri badala ya saa 10:30 alasiri kama kanuni zinavyotaka.

Katika hatua nyingine, Meneja wa Yanga, Walter Harson, amefungiwa michezo mitatu pamoja na kutozwa faini ya Sh milioni moja kwa kosa la kumsukuma mchezaji wa Simba, Clatous Chama, wakati wa mchezo huo.

Leave a Comment