
Rais wa Yanga SC, Eng. Hersi Ally Said, ameongoza kikao maalumu kilichojadili mustakabali wa mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Klabu hiyo katika Makao Makuu ya Jangwani, Dar es Salaam.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Ghalib Said Mohammed (GSM), Rais wa GSM Group of Companies, ambaye ni mbia mkuu na mshindi wa zabuni ya ujenzi wa uwanja huo wa kisasa.
Baada ya kikao hicho, viongozi wa klabu wakiongozwa na Rais Eng. Hersi Ally Said pamoja na GSM walitembelea eneo lililopangwa kujengwa uwanja huo ili kujionea hali ya eneo na maandalizi ya awali ya mradi huo mkubwa wa maendeleo ya miundombinu ya klabu.



