
Fainali ya Kombe la FA natarajiwa kuchezwa leo Jumamosi katika uwanja wa Wembley Stadium, ambapo miamba miwili ya soka nchini England itakutana katika pambano lenye mvuto mkubwa na presha ya hali ya juu.
Mechi hiyo itawakutanisha Chelsea dhidi ya Manchester City, timu mbili zenye historia kubwa na ushindani wa mara kwa mara katika soka la England.
Kwa upande wa Manchester City, kocha Pep Guardiola na kikosi chake wanaingia uwanjani wakiwa na lengo la kumaliza msimu kwa heshima baada ya changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwenye baadhi ya michezo mikubwa. City wamejijengea sifa ya umiliki mkubwa wa mpira, pressing ya kasi na ushindani wa mara kwa mara katika mataji, lakini msimu huu wamekumbana na ushindani mkali zaidi kuliko kawaida.
Tengeneza pesa leo kwenye michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile Keno, Aviator, Poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Hivyo, FA Cup imekuwa muhimu kwao kama nafasi ya kuthibitisha kuwa bado wana nguvu na ubora wa kubeba mataji makubwa nchini England.
Kwa upande wa Chelsea, mchezo huu unaweza kuwa muhimu sana katika safari yao ya kujijenga upya. Baada ya kipindi cha mabadiliko ya mara kwa mara ya makocha na usajili mkubwa, klabu hiyo inaanza kuonyesha dalili za kurudi kwenye ushindani wa juu kupitia kikosi chenye wachezaji vijana na wenye uwezo mkubwa.
Ushindi katika fainali hii dhidi ya Manchester City unaweza kuwa ujumbe muhimu kwamba Chelsea wameanza kurejea kwenye ubora wao wa kihistoria.
Takwimu zinaonyesha kuwa timu hizi zimekutana zaidi ya mara 180 katika mashindano yote, zikiwa na ushindani mkali na karibu sawa katika matokeo ya jumla, jambo linaloifanya mechi hii kuwa ya kusisimua zaidi.
Mashabiki wanatarajiwa kushuhudia pambano lenye kasi, mbinu na presha kubwa, huku kila timu ikisaka kutwaa taji hili la heshima katika moja ya viwanja maarufu zaidi duniani.