
Meli kubwa ya kivita ya Marekani, USS Gerald R. Ford, imerejea rasmi katika kituo chake cha kijeshi Norfolk, Virginia baada ya kukamilisha safari ya miezi 11 baharini, moja ya safari ndefu zaidi tangu enzi za Vita vya Vietnam.
Safari hiyo ilihusisha operesheni muhimu katika maeneo yenye mvutano kama Bahari ya Mediterranean, Mashariki ya Kati na Bahari ya Arabia, ikilenga kuimarisha usalama na kulinda njia za biashara duniani.

Mamamia ya ndugu na jamaa walijitokeza kuwapokea wanajeshi waliorejea, huku hisia kali zikionekana baada ya karibu mwaka mzima wa kutengana.
Licha ya mafanikio ya kijeshi, safari hiyo imeibua mjadala kuhusu athari za kisaikolojia kwa wanajeshi kutokana na muda mrefu waliotumia baharini katika mazingira ya tahadhari kubwa.
Jeshi la Marekani limesifu kikosi hicho na linatarajiwa kufanya tathmini ya kina kuhusu safari hiyo na athari zake kwa operesheni zijazo.
