
Nyota wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo, ameendelea kusubiri taji rasmi akiwa na Al Nassr FC baada ya klabu hiyo kupokea kipigo cha 1-0 dhidi ya Gamba Osaka katika fainali ya michuano ya AFC Champions League Two iliyopigwa kwenye dimba la Al Awwal Park mjini Riyadh, Saudi Arabia.
Bao pekee la mchezo lilifungwa dakika ya 30 na mshambuliaji Hummet aliyewapa Gamba Osaka ushindi muhimu na ubingwa wao wa kwanza kabisa wa mashindano hayo ya bara Asia.

Matokeo hayo yanaendelea kuongeza presha kwa Ronaldo ambaye bado hajafanikiwa kubeba taji kubwa akiwa na Al Nassr tangu alipojiunga na klabu hiyo mwishoni mwa mwaka 2022.
Hata hivyo, matumaini bado yapo kwa Al Nassr kumaliza msimu kwa furaha kwani klabu hiyo inaongoza msimamo wa Saudi Pro League na inahitaji ushindi katika mchezo wa mwisho wa ligi ili kujihakikishia ubingwa wa msimu huu.
FT: Al Nassr FC 🇸🇦 0-1 🇯🇵 Gamba Osaka
⚽ 30’ Hummet
