×

Rio Ferdinand Atua Tanzania Kwa Ziara Maalum ya Siku Nne – (Video + Video)

Nyota wa zamani wa Manchester United F.C. na timu ya taifa ya England, Rio Ferdinand, amewasili nchini Tanzania leo Jumanne, Mei 19, 2026 kwa ziara ya siku nne itakayomalizika Mei 22, 2026.

Ferdinand anakuja nchini kwa mwaliko maalum wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, katika ziara inayolenga kukuza michezo, utalii na fursa za kiuchumi kupitia sekta ya michezo.

Kupitia video iliyosambaa mitandaoni, Ferdinand amesema ziara yake inazingatia watu, utamaduni na fursa zilizopo Tanzania, akieleza kuvutiwa na shauku kubwa ya vijana wa Kitanzania katika michezo hasa soka.

Amesema pia anatarajia kukutana na viongozi mbalimbali wa serikali, ikiwemo Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ili kujadili namna ya kuendeleza fursa za michezo na maendeleo ya vijana.

Ujio wa Ferdinand unatazamwa kama fursa muhimu kwa Tanzania katika kutangaza utalii wake, kukuza uwekezaji katika michezo na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya michezo na vijana.

Leave a Comment