
Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetangaza rasmi nafasi kubwa za ajira 309 katika taasisi mbalimbali za serikali na mashirika ya umma nchini Tanzania.
Tangazo hilo linahusisha nafasi za kazi katika taasisi kama vile Mzumbe University (MU), Ardhi University (ARU), Moshi Co-operative University (MoCU), e-Government Authority (eGA), Tanzania Railways Corporation (TRC), Tanzania Government Flight Agency (TGFA) na National Arts Council (NAC) pamoja na taasisi nyingine za umma.
Fursa hizi mpya za ajira zinahusisha kada mbalimbali zikiwemo:
- ICT Officers katika maeneo ya Programu, Mitandao, Database na Helpdesk
- Wahandisi, Mafundi na Wataalamu wa Ufundi
- Madereva, Wasaidizi wa Ofisi na Mapokezi
- Wataalamu wa Reli, Anga na Usafirishaji
- Wataalamu wa Sanaa na Utamaduni
NAFASI ZA KAZI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA 19-05-2026
PSRS imesisitiza kuwa waombaji wote wanatakiwa kutuma maombi yao kupitia mfumo rasmi wa ajira wa serikali kupitia http://portal.ajira.go.tz kabla ya tarehe ya mwisho ya 01 Juni 2026.
Waombaji wanakumbushwa kuwasilisha nyaraka sahihi, zikiwemo vyeti vya elimu, kitambulisho cha taifa (NIDA), na taarifa nyingine muhimu kama ilivyoelekezwa kwenye tangazo rasmi.
PSRS imeeleza kuwa waombaji wote wenye sifa wanahimizwa kuchangamkia fursa hii adimu ya ajira serikalini, huku ikisisitiza kuwa maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo rasmi hayatazingatiwa.
MUHIMU:
Mwisho wa kutuma maombi: 01 Juni 2026