×

Rais wa Syria Amshukuru Trump kwa Zawadi ya Manukato ya Bei Kubwa

Rais wa Syria Ahmed Al-Sharaa amemshukuru Rais wa Marekani Donald Trump kwa kumtumia zawadi ya manukato ya bei kubwa ya chapa ya Trump, hatua iliyozua mjadala mkubwa mitandaoni kuhusu mahusiano mapya kati ya Syria na Marekani.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X, Sharaa alisema:

“Baadhi ya mikutano huacha kumbukumbu; wetu umeacha harufu.”

Ujumbe huo uliambatana na picha ya boksi mbili za manukato ya Trump  moja nyekundu na nyingine nyeusi pamoja na ujumbe maalum kutoka kwa Trump uliosomeka:

“Watu wote bado wanazungumzia picha tuliyopiga nilipokupa manukato haya mazuri  endapo yamekwisha!”

Tukio hilo linaendelea kuvuta hisia tangu mkutano wa kihistoria kati ya viongozi hao uliofanyika Ikulu ya Marekani mwezi Novemba mwaka jana, ambapo Trump alimpa Sharaa manukato hayo mbele ya kamera na hata kumpulizia moja kwa moja.

Katika mkutano huo, Trump pia alimkabidhi Sharaa boksi la manukato kwa ajili ya mke wake huku akifanya mzaha kwa kumuuliza ana wake wangapi.

Manukato hayo ya chapa ya Trump yanauzwa kwa dola 249 (Tsh 649, 891) kwa chupa moja na yanaelezwa na kampuni hiyo kuwa yanaashiria “nguvu, mamlaka na ushindi.”

Tangu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa Syria Bashar Assad mwaka 2024, serikali mpya ya Syria chini ya Ahmed Al-Sharaa imeanza kufungua ukurasa mpya wa mahusiano na Marekani.

Utawala wa Trump umeondoa baadhi ya vikwazo dhidi ya Syria na kuanza kushirikiana kwa karibu zaidi na Damascus kwa ushawishi wa Saudi Arabia na Uturuki, licha ya wasiwasi kutoka Israel.

Mkutano wa kwanza kati ya Trump na Sharaa ulifanyika Saudi Arabia mwaka jana ambapo Trump alimuelezea kiongozi huyo wa Syria kama “kijana mwenye mvuto.”

MELI KUBWA MBILI za MAFUTA za CHINA ZAPENYA HORMUZ BAADA ya KUKWAMA kwa MIEZI MIWILI….📍IRAN

Leave a Comment