×

Rio Ferdinand Apongeza Viwango vya Kimataifa vya Uwanja wa Arusha

 

Nyota wa zamani wa mpira wa miguu wa timu ya Taifa ya Uingereza na Klabu ya Manchester United Rio Ferdinand amesema, Uwanja wa Arusha ambao utatumika katika Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2027 (AFCON 2027) umejengwa kwa kiwango bora kilichozingatia viwango vya kisasa duniani.

Amesema hayo Mei 21, 2026 wakati alipotembelea uwanja huo,ikiwa ni muendelezo ziara yake hapa nchini, hususani jijini Arusha ambapo aliongozana na mwenyeji wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Paul Makonda.

“Nimecheza kwenye viwanja vingi duniani lakini kiwanja hiki ni kizuri na chenye viwango, niwapongeze wajenzi, wakandarasi na watalaam wote wanaofanya kazi hii nzuri” alisema Rio.

Ameweka bayana furaha yake na kufurahisha na namna alivyopokelewa na kukaribishwa na Watanzania akiahidi kurudi tena.

Rio amesifu namna alivyokaribishwa na watanzania akisema haijawahi kutokea kokote alikotembelea duniani. Ameisitiza kuwa amekaribishwa kwa tabasamu na upendo mkubwa, chakula ni kizuri na mambo mengi ya watanzania ni mazuri.

 

Leave a Comment