×

Video: Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Awaka Kisa Matukio ya Utekaji Nchini

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amekemea vitendo vya utekaji akieleza kuwa ni njama na michezo ya kuwagombanisha wananchi na serikali yao.

Dkt. Mwigulu amesema hayo Mei 23, 2026 alipozungumza na wananchi wa Manispaa ya Iringa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.

Amesema amani ni msingi wa maendeleo ya Taifa na kwamba Watanzania wanapaswa kuendelea kulinda mshikamano wa kitaifa na kukataa vitendo vya uchochezi vinavyoweza kusababisha migawanyiko ya kisiasa, kidini au kijamii.

Aidha, Dkt. Mwigulu amesema zipo njama mbalimbali zinazolenga kuwagombanisha Watanzania kupitia siasa, dini na taarifa za upotoshaji huku akiwataka wananchi kuwa makini na watu wanaowachochea kufanya vitendo vinavyohatarisha usalama wa nchi.

🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.

Leave a Comment