
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Allan Okello ametangazwa kuwa nyota wa mchezo baada ya kuiongoza timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa kwenye dimba la KMC Complex.
Nyota huyo raia wa Uganda aliifungia Yanga mabao mawili dakika ya 52 na 85 huku bao jingine likifungwa na Abuya dakika ya 26, wakati Namungo wakipata bao lao kupitia Kabunda dakika ya 40.
Kwa ushindi huo, Okello ameifikishia Yanga mchango wa mabao 18 tangu ajiunge na klabu hiyo Januari 2026, akiwa amefunga mabao 11 na kutoa asisti 7 kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Matokeo kamili:
FT: Yanga SC 3-1 Namungo FC
⚽ 26’ Abuya
⚽ 40’ Kabunda
⚽ 52’ Okello
⚽ 85’ Okello
Msimamo wa juu wa ligi kwa sasa:
- Yanga SC — mechi 25 — pointi 60
- Simba SC — mechi 25 — pointi 58