×

FIFA Yatangaza Rasmi Uwanja wa Ufunguzi wa Kombe la Dunia 2026

Kombe la Dunia 2026 litaanza rasmi tarehe 11 Juni 2026 huku mchezo wa ufunguzi ukipigwa katika Uwanja wa Mexico City, jijini Mexico City.

Uwanja huo utaandika historia kwa kuwa wa kwanza duniani kuandaa mechi tatu za ufunguzi za Kombe la Dunia, baada ya pia kufanya hivyo mwaka 1970 na 1986.

Mashindano ya mwaka 2026 yatakuwa makubwa zaidi kuwahi kufanyika, yakishirikisha timu 48 na jumla ya mechi 104 zitakazochezwa katika miji 16 ndani ya nchi tatu ambazo ni Mexico, Canada na United States.

Wenyeji Mexico watafungua pazia la mashindano hayo nyumbani kwao kabla ya kucheza michezo mingine miwili ya hatua ya makundi katika viwanja vyao vya nyumbani, ikiwemo mchezo mmoja katika Estadio Guadalajara.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, Mexico City Stadium wenye uwezo wa kubeba mashabiki 83,000 pia utaandaa mchezo wa Kundi K kati ya Uzbekistan na Colombia pamoja na michezo ya hatua ya Round of 32 na Round of 16.

Leave a Comment