×

Global TV Online Yatangaza Nafasi ya Kazi ya Content Moderator

GLOBAL TV imetangaza nafasi ya kazi kwa vijana wenye ubunifu na shauku ya kufanya kazi kwenye sekta ya habari za kidigitali.

Kampuni hiyo inatafuta mtu wa kujaza nafasi ya Content Moderator atakayekuwa sehemu ya timu ya kidigitali katika ofisi zao zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

Sifa zinazohitajika:

  • Awe mhitimu wa chuo au chuo kikuu
  • Awe na uzoefu wa kuandika na kutengeneza maudhui kwa mitandao ya kijamii kama Instagram, Facebook, TikTok na X
  • Awe na uzoefu mkubwa wa kutumia AI katika utengenezaji wa maudhui na usimamizi wa mitandao ya kijamii
  • Awe na ujuzi mzuri wa kutumia kompyuta na simu janja
  • Awe na uwezo mzuri wa kuzungumza na kuandika Kiswahili pamoja na Kiingereza
  • Awe mkazi wa Dar es Salaam
  • Awe mbunifu, mwenye hamu ya kujifunza na uwezo wa kufanya kazi chini ya presha

Mahali pa kazi:

Global Group House, Sinza Mori, Dar es Salaam.

Jinsi ya kutuma maombi:

Waombaji wanatakiwa kutuma CV zao kupitia barua pepe:
[email protected]

Kwa mawasiliano zaidi:
📞 +255 799 444 036

Leave a Comment