×

Jasinta Makwabe Avutiwa na Usafi wa Kigali na Nidhamu ya Rwanda

Mwanamitindo na mjasiriamali wa Tanzania, Jasinta Makwabe, amefunguka kuhusu mambo yaliyomvutia zaidi alipowasili nchini Rwanda, akitaja usafi wa jiji la Kigali pamoja na nidhamu ya vyombo vya usalama kutokudai rushwa kutoka kwa wananchi kuwa ni vitu vilivyomshangaza kwa kiwango kikubwa.

Jasinta amesema hali hiyo ni tofauti na baadhi ya mataifa mengine aliyowahi kuyatembelea, akieleza kuwa mazingira ya Kigali yanaonyesha kiwango kikubwa cha utaratibu, usalama na uwajibikaji

. Aidha, baadhi ya wageni pamoja na watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakisifia Rwanda kwa usafi wake pamoja na hali ya amani na usalama, hasa katika jiji la Kigali.

Mwanamitindo huyo ambaye kwa sasa yupo Kigali kuhudhuria michezo ya fainali ya Basketball Africa League Finals, alitoa kauli hiyo kupitia mahojiano aliyofanya na IGIHE ambapo alieleza namna alivyoona utofauti mkubwa wa maisha ya kila siku nchini humo ukilinganisha na maeneo mengine aliyowahi kufika.

Leave a Comment