
Dunia inaenda kushuhudia pambano la aina yake kabisa kwenye Fainali ya Ligi ya Mabingwa kule Ulaya ni PSG vs Arsenal. Timu kutoka majiji mawili yaani Paris na London. Vita ya walimu Luis na Mikel Arteta. Ushindi unampa nani leo?
Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kati ya PSG dhidi ya Arsenal unatarajiwa kupigwa Jumamosi hii kule Hungary ambapo huu ni mchezo ambao umebeba hisia za mashabiki wengi Duniani kutoka na timu ambazo zinakutana, kwani kwa Arsenal, ni nafasi ya kurejesha heshima yao katika soka la Ulaya na hatimaye kutwaa taji ambalo limekuwa ndoto kwa miaka mingi.
Wakati PSG wao wakiwa kama mabingwa watetezi wanaingia katika fainali hii wakiwa na kujiamini kubwa sana. Msimu mzima wameonyesha ubora mkubwa wa kushambulia, kasi ya mchezo na uwezo wa kuua mechi ndani ya dakika chache. Safu yao ya ushambuliaji imekuwa tishio kwa kila timu waliokutana nayo, na mara nyingi wameonekana kuwa na uwezo wa kubadili matokeo hata wanapokuwa chini ya presha. Beti hapa.
Arsenal wao wamefika hatua hii kupitia safari ya uvumilivu na nidhamu kubwa. Tofauti na PSG wanaopenda kucheza kwa kasi ya juu, Arsenal wameonyesha uwezo mkubwa wa kusimamia mechi kwa utulivu. Mikel Arteta ameijenga timu inayocheza kwa mpangilio mkubwa, inayojua lini kushambulia na lini kujilinda.
Piga pesa leo kwenye michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile Keno, Aviator, Poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
The Gunners wakiwa kama mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza yaani EPL wamekuwa timu ngumu sana kufungwa, na hilo linaweza kuwa silaha yao kubwa zaidi katika fainali hii. Wachezaji wao wameonyesha moyo mkubwa wa kupambana na hali hiyo imewarudisha kwenye hadhi ya timu kubwa Ulaya. Meridianbet wameweka ODDS KUBWA mechi hii. Suka jamvi hapa.
Mchezo huu unaweza kuamuliwa zaidi na namna timu zitakavyokabiliana na presha. Katika fainali, si kila mara ubora wa kiufundi pekee unaoshinda. Mara nyingi kinachobeba timu ni utulivu wa akili na uwezo wa kutumia nafasi muhimu. PSG wana uzoefu mkubwa zaidi wa kucheza mechi za kiwango hiki katika miaka ya karibuni, lakini Arsenal wanaonekana kuwa na njaa kubwa zaidi ya ushindi. Hiyo inaweza kufanya mchezo huu kuwa mgumu kutabiri.
Kitu kingine kinachofanya fainali hii kuwa ya kusisimua ni mapambano ya kiufundi kati ya makocha wawili wenye falsafa tofauti kabisa. Luis Enrique anapenda timu yake icheze kwa uhuru mkubwa wa kushambulia na kutumia ubunifu wa wachezaji wake wa mbele. Arteta yeye hupenda udhibiti wa mchezo, presha ya pamoja na mpira kusogezwa kwa utaratibu. Hivyo, ndani ya dakika 90 mashabiki wanaweza kushuhudia vita ya mbinu kati ya kasi ya PSG na utulivu wa Arsenal.