Wimbo mpya wa Harmonize akimshirikisha Chile One wa Zambia uitwao “Hichilema” umeendelea kuvuta hisia kubwa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika baada ya kutoka rasmi wiki hii.
Video hiyo inaelezwa kuwa ya kizalendo na ya kuhamasisha umoja, huku ikimpongeza Rais wa Zambia Hakainde Hichilema kwa uongozi wake. Pia imechanganya ladha ya Bongo Flava kutoka Tanzania na muziki wa kisasa wa Zambia.