
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameshiriki ibada ya Jumapili, leo, Mei 31, 2026, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kati, Usharika wa Manyoni, wilayani Manyoni, mkoani Singida.
Ibada hiyo imeongozwa na Mkuu wa Jimbo la Kusini, Mchungaji Anton Issingo kwa kushirikiana na Mchungaji wa KKKT Usharika wa Manyoni, Elia Kisuda.
Pamoja na Waziri Mkuu Mwigulu, pia ibada hiyo imehudhuriwa na viongozi wengine wa Serikali, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego.
