
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ismani, Emmanuela Mtatifikolo ametangazwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika Juni 1, 2026 baada ya kupata kura 70,905 sawa na asilimia 93.5 ya kura zote zilizopigwa.
Matokeo hayo yametangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu kura katika jimbo hilo.
Uchaguzi huo umefanyika katika Tarafa za Ismani, Idodi na Pawaga, huku jumla ya kata 13 na vijiji 60 vikishiriki kwenye mchakato mzima wa uchaguzi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, wananchi 76,556 sawa na asilimia 85 ya wapiga kura waliojiandikisha walijitokeza kushiriki uchaguzi huo.
Katika uchaguzi huo wa Jimbo la Ismani, Emmanuela Mtatifikolo wa Chama Cha Mapinduzi alikuwa anashindana na wagombea kutoka vyama 16 tofauti vya siasa.
Baadhi ya vyama vilivyoshiriki ni:
- Chama Cha Mapinduzi (CCM)
- CUF
- NCCR-Mageuzi
- UDP
- ADC
- TLP
- CHAUMMA
- UPDP
- DP
- CCK
- SAU
- ADA-TADEA
- NLD
- UMD
- AAFP
- MAKINI
- NRA
Jumla ya wagombea 17 walishiriki katika uchaguzi huo mdogo wa ubunge