×

Zaiylissa Amuonya Dulla Makabila Kumtaja Kwenye Mahojiano “Nimechoka” -Video

Muigizaji Zaiylissa

Muigizaji Zaiylissa amempa onyo kali msanii wa Singeli Dulla Makabila, akimtaka kuacha kabisa kumzungumzia kwenye mahojiano mbalimbali (interviews) na kuheshimu ndoa yake.

Kupitia ujumbe aliouandika mitandaoni, Zaiylissa amesema amekuwa kimya kwa muda licha ya mambo anayodai kufanywa na Dulla Makabila, lakini sasa ameamua kuweka msimamo wake wazi na kumtaka aache kabisa tabia hiyo.

Amesema amechoka na anataka kuachwa kwa amani, akisisitiza kuwa yeye ni mke wa mtu na anahitaji kuheshimiwa katika ndoa yake.

Aidha, ametoa onyo kali akimwambia Dulla Makabila asimzungumzie tena kwenye interviews zake wala kumtaja kwenye mitandao ya kijamii.

Msanii wa Singeli Dulla Makabila

Leave a Comment