×

Fahamu Kicheche: Mnyama Mdogo Mwenye Tabia za Kuvutia

Kicheche ni mnyama mdogo jamii ya Nguchiro wanaopatikana sehemu mbalimbali duniani. Wanyama hawa hutofautiana mwonekano kutokana maeneo walipo lakini kimsingi tabia zao wote hufanana.

Kicheche ndiye mnyama malaya zaidi kuliko mnyama yeyote yule duniani. Umalaya wake unatokana na kuwa kinara wa kufanya ngono mara nyingi zaidi kila siku kuliko mnyama wa aina yeyote ile.

Kwa kawaida Kicheche jike anapokutana na dume kitu cha kwanza kabisa kumpa ni kuhakikisha anafanya naye ngono, kisha wanapomaliza ndiyo huenda kula.

Tabia hii ya Kicheche jike humsababishia kufanya ngono na kila dume anayekutana naye, huku ikikadiriwa kwa siku moja mnyama huyo hufanya ngono zaidi ya mara 60 na madume tofauti tofauti.

Ukubwa huu unasababishwa na wastani wake wa kutembea umbali mrefu zaidi wakati wa kufanya shughuli mbalimbali za kutafuta chakula nk. Inakadiriwa Kicheche hutembea umbali wa kilomita 360 kwa siku.

Huko njiani Kicheche jike anapokutana na madume lazima ahakikishe anawapa ngono kwanza kabla ya salamu, kisha wanapomaliza hujitafutia chakula. Na ndio maana wasichana Malaya huitwa vicheche.

Pamoja na Kicheche kuwa na sifa ya umalaya na mwonekano mzuri, mnyama huyo anatajwa kuwa ndiye mnyama anaongoza kutoa harufu kali na mbaya zaidi kuliko mnyama mwingine yeyote duniani.

Harufu hiyo kali ya Kicheche hutumika kama silaha ya kumkinga na wanyama maadui wanaotaka kumdhuru. Inaelezwa kuwa wanyama hao wanapojaribu kumsogelea huachia harufu hiyo kali inayowafanya wote kukimbia mbali.

Kicheche hula ndege, wanyama wadogo, wadudu, na hata kula baadhi ya matunda, japo naye huliwa na wanyama wakiwemo Nyoka, Ndege aina ya Tai na hata baadhi ya wanyama wengine wanaokula nyama.

Moja kati ya mbinu yake maarufu ya kukamata viumbe wadogo kama kuku, ni kuweka chakula kinachopendwa na ndege hao sehemu zake za nyuma, huku akiuficha mwili wake kwenye majani na kuinua mkia wake juu.

Ndege wanapoona chakula hicho na kukisogelea ili kula, mnyama huyo hutumia mkia wake kumpiga pigo la nguvu ndege huyo na kisha hugeuka haraka kumkamata kwa vidole vyake vyenye kucha kali na kuanza kumla.

Makala na Elvan Stambuli, Global Digital

Leave a Comment