×

Hospitali ya Ebola Yateketezwa Baada ya Kisa cha Kijana Kufariki

Umati wenye hasira umechoma moto sehemu ya hospitali inayowahudumia wagonjwa wa Ebola mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kufuatia tukio la familia na marafiki wa kijana aliyefariki kuvamia hospitali hiyo na kuchukua mwili wake kwa nguvu kwa ajili ya mazishi.

Kwa mujibu wa taarifa, watu hao walianza kurusha mawe na kuchoma mahema yaliyokuwa yakitumika kama wodi za kuwahifadhi wagonjwa waliotengwa, hatua iliyosababisha taharuki kubwa katika eneo hilo.

Mamlaka za afya zinasisitiza kuwa miili ya watu waliokufa kutokana na Ebola huwa na hatari kubwa ya kueneza ugonjwa huo, hivyo taratibu maalum za mazishi salama hufuata ili kuzuia maambukizi zaidi.

Tukio hilo limetokea katika hospitali ya Rwampara, iliyoko karibu na mji wa Bunia katika jimbo la Ituri, ambako visa vingi vya Ebola vimeripotiwa.

Kutokana na hali hiyo, wahudumu wa afya wamelazimika kuwekwa chini ya ulinzi wa jeshi huku polisi wakijaribu kurejesha utulivu.

Inaelezwa kuwa kijana huyo alikuwa maarufu katika jamii, jambo lililochangia hasira za wananchi ambao bado wana uelewa mdogo kuhusu hatari ya ugonjwa wa Ebola.

TRUMP AKIRI KUZOZANA na NETANYAHU HADI KUMWITA KICHAA – “ALINIKERA SANA” – ADAI ni RAFIKI YAKE MZURI

Leave a Comment