×

Je, Soko la Tanzania Liko Tayari Kwa Ubunifu wa Kiwango cha Dunia?

Kwa miaka mingi, chapa nyingi nchini Tanzania zipo kila mahali lakini ni ngumu mtu kuzikumbuka. Nembo kubwa jukwaani, DJ’s maarufu, vinywaji kwa bei nafuu, na watengeneza maudhui wa mitandoni wakituma video zisizofikisha ujumbe kamili kwenye mitandao ya kijamii ( Instagram). Baada ya hapo, kila mtu anarudi nyumbani kwake, hadi kufikia jumatatu tukio lote limesahaulika.

Huo umekuwa ni ukweli mchungu kwa chapa nyingi zaidi barani Afrika. Kampuni inatumia fedha nyingi zaidi kujitangaza, lakini hushidwa kuacha historia isiyofutika kwa wateja na walaji wake. Kibaya zaidi, walaji nao wamegundua hilo.

Siku hizi, watumiaji wana ladha tofouti. Hawavutiwi tena na uwepo wa chapa ya kampuni peke yake, bali ubunifu uliopo nyuma ya uwepo wa chapa hiyo.

Ndiyo maana, tukio walilolifanya Heineken hivi karibuni la Kuonesha fainali za ligi ya Mabingwa barani Ulaya limeacha historia ya kipekee. Tukio hilo liliibua gumzo kitaifa, sio kwa sababu ya mpira wa miguu tu, bali ni kwa sababu ilionesha kiwango kikubwa cha fursa ambazo bado watu wengi hawajazijua katika kubadilisha namna tunavyotengeneza burudani kwa watumiaji wetu nchini Tanzania.

Kwa usiku mmoja watanzania walipewa burudani kubwa yenye hadhi ya Kimataifa, yenye mvuto wa kisasa na mazingira yaliyobuniwa kwa hali ya juu na kukosha mioyo ya walaji wengi. Muonekano wa eneo lenyewe ilikuwa ni kivutio tosha. Makontena yaligeuka kuwa chanzo cha kivutio, ubunifu wa njia za juu uliwashangaza maelfu ya watu waliohudhuria. Skrini kubwa ilitawala na kufananisha uwoneshaji wa fainali hizo na tamasha kubwa la muziki kimataifa.

Watu hawakuhudhuria tu bali walishiriki historia.

Tofouti hiyo ni muhimu sana, kwa sababu inawafanya walaji kujisikia umuhimu sana kuwepo katika tukio hilo kubwa. Kwa sababu hiyo itabaki kama historia kwenye maisha yao na sehemu ya utambulisho wao. Watu wanapenda kushiriki matukio yanaoakisi utu wao wa ndani, na mtindo wa maisha wanaoutamani.

Hali hii inaonekana zaidi kwa vijana wa mijini ambao sasa wanaishi katika ulimwengu uliounganishwa kidijitali. Wanatazama maisha ya usiku ya Lagos kupitia TikTok. Wanafuatilia tamasha za Amsterdam au London kupitia Instagram. Kila siku wanakutana na viwango vya kimataifa vya ubunifu na mandhari ya kisasa. Matarajio yao yamebadilika sana zaidi ya chapa za kampuni nyingi walipofikia.

Hata hivyo kuna Chapa za Kampuni nyingi zaidi bado zinafanya kazi zikiwa na maono ya 2015. Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na dhana ya kwamba walaji wengi wa Afrika Mashiriki hawaitaji utekelezaji wa kiwango cha Kimataifa. Ndio maana wanafanya uzalishaji mdogo, ubunifu mdogo, miundombinu ya kawaida na sauti zisizoridhisha. Nembo za chapa ya kampuni kila mahali bila kuwa na hadithi ya kusimulia. Kauli yao maarufu huwa ni kuwa  “hiki kinatosha kwa soko letu”.

Lakini, pengine soko halikuwa tatizo hata siku moja, huenda tatizo lilikuwa ni ukosefu wa Ubunifu.

Kwa sababu mwitikio ulioonekana siku ile ulithibisha jambo moja muhimu ambalo ni wananchi wana kiu na ubunifu wa viwango, wanataka vitu vipya, muonekano unaovutia na mradi utekelezwe kwa viwango vinavyohitajika.

Mitandao ya kijamii ililipuka kwa maudhui ya video. Video za drone zilisambaa kila mahali. Watu hawakushiriki tu mechi yenyewe, bali walionyesha mazingira, usanifu wa eneo, nguvu ya umati na ukubwa wa tukio. Hata watu ambao hawakuwa mashabiki wakubwa wa mpira walitamani kuhudhuria kwa sababu mazingira yenyewe yalikuwa kivutio cha kitamaduni.

Hilo linapaswa kuwafanya wataalamu wa masoko wengi kutafakari! Kwa sababu linaashiria mabadiliko makubwa katika namna walaji wanavyohusiana na chapa. Kwa sasa, uzoefu wenyewe unaanza kuwa bidhaa. Si kinywaji, si tiketi wala si udhamini bali ni uzoefu wenyewe. Na hapo ndipo chapa nyingi zinaanza kupoteza umuhimu wake.

Bajeti nyingi za masoko bado zimejikita katika kupima kiwango cha mwonekano badala ya athari za kihisia. Aktivisheni nyingi bado zinaundwa kwa lengo la kuridhisha ripoti za ‘PowerPoint’ na taratibu za manunuzi, badala ya kuunda nyakati ambazo watumiaji watazikumbuka kwa miaka mingi.

Matokeo yake ni sekta yenye matukio makubwa kwa ukubwa, lakini matupu kihisia. Yenye watu wengi, lakini yasiyokumbukwa.

Watumiaji wanaweza kutambua tofauti hiyo mara moja. Wanajua chapa inapojaribu kwa dhati kuunda utamaduni mpya na wanajua inapojaribu tu kujitangaza ndani ya utamaduni uliopo.

Ndiyo maana uzoefu huu wa Heineken ulipokelewa vizuri sana. Ulionekana kuwa wa makusudi. Uliundwa kwa umakini. Uliandaliwa kwa viwango vya juu. Uliwatendea watumiaji kama watu wanaostahili uzoefu wa kiwango cha kimataifa, si kama jambo la mwisho kufikiriwa.

Lakini hadhira ya leo haitoi tu pongezi kwa jitihada. Inatambua na kuthamini ubora. Na hilo linabadilisha kila kitu.

Kwa sababu mara tu watumiaji wanapopata uzoefu wa mazingira ya kuvutia, ya kiwango cha juu na yenye kuamsha hisia, huwa ni vigumu  kuridhika tena na aktivisheni za kawaida zilizojaa viti vya plastiki, msongamano wa watu, mifumo dhaifu ya sauti na mbinu zilezile zinazojirudia kila mwaka.

Kiwango kimepandishwa rasmi, na chapa ambazo zitashindwa kutambua mabadiliko haya zinaweza kuanza kupotea polepole katika mazungumzo ya kitamaduni na kijamii.

Hili si suala la burudani pekee. Ni suala la mustakabali wa masoko. Chapa zitakazoongoza katika miaka kumi ijayo si lazima ziwe zile zenye bajeti kubwa zaidi za matangazo bali zitakuwa zile zinazoweza kujenga ulimwengu ambao watu wanatamani kuwa sehemu yake.

Mustakabali ni wa chapa zinazoelewa umuhimu wa mazingira, simulizi, hisia na kujenga jamii zinazowaunganisha watu. Chapa zinazokoma kuingilia utamaduni na badala yake kuanza kuutengeneza.

Hicho ndicho kilichoufanya uzoefu huu kuwa wa kipekee. Kwa usiku mmoja, ulizipa changamoto dhana zilizokuwepo kwa muda mrefu kuhusu kile ambacho hadhira ya Tanzania inapaswa kutarajia kutoka kwa matukio ya hapa nchini. Ulionyesha wazi kwamba soko hili liko tayari kwa mawazo makubwa, ubunifu wa kiwango kikubwa na utekelezaji unaoweza kushindana na viwango vya kimataifa.

Na pengine ndiyo sababu mjadala wake ulisambaa kwa haraka kote nchini. Si kwa sababu watu walikuja kutazama mpira wa miguu, bali kuona taswira ya kile ambacho uzoefu wa chapa nchini Tanzania unaweza kuwa pale ambapo ubunifu unapopewa nafasi yake stahiki.

Swali la msingi sasa ni hili:

Je, chapa nyingine ziko tayari kuwa jasiri vya kutosha kufuata njia hiyo?

Leave a Comment