
Baada ya kupata mtoto wa kiume, Wema Sepetu ameandika ujumbe wa kugusa hisia akimshukuru Mungu pamoja na mpenzi wake, Whozu, kwa hatua hiyo kubwa katika maisha yao.
“Mungu ndiye Power, katupendelea… Yee kasema sawa, tulichongojea…”
Wema amesema kuwa Mungu amewajibu maombi yao kwa wakati wake, jambo ambalo limewaletea furaha kubwa baada ya kipindi kirefu cha kusubiri.
“Asante baba mtoto wangu… Mungu wetu ni mkali na ametujibu kwa wakati… Tuzidi kumtukuza na kumuabudu… Hakika tuliomba sana na ametushangaza…”
Ujumbe huo umeendelea kuwagusa mashabiki wengi ambao wamekuwa wakifuatilia safari yake ya kutimiza ndoto ya kuwa mama, huku wengi wakieleza kuwa ni ushuhuda wa imani, subira na kutokukata tamaa.
