×

Brenda Rupia Afafanua Hoja ya Katiba Mpya Nchini “Ni Matakwa ya Wananchi” – Video

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Brenda Rupia.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Brenda Rupia amesema kuwa suala la katiba mpya halipaswi kuonekana kama ajenda ya chama kimoja, bali ni matakwa ya wananchi wote wa Tanzania.

Akizungumza kupitia kipindi cha Front Page kinachorushwa na Global TV pamoja na 255 Global Radio, Brenda alisema mjadala wa katiba mpya una maslahi mapana ya kitaifa na unagusa mustakabali wa demokrasia nchini.

Ameeleza kuwa ni muhimu kwa wadau wote wa siasa, pamoja na wananchi wa kawaida, kushiriki kikamilifu katika kuendelea kuibua na kuunga mkono mjadala huo ili kufikia katiba bora itakayowakilisha matakwa ya Watanzania wote.

Kauli hiyo imekuja wakati mjadala wa katiba mpya ukiendelea kuchukua nafasi kubwa katika ajenda za kisiasa nchini, huku wadau mbalimbali wakiendelea kutoa maoni tofauti kuhusu mchakato wake.

Leave a Comment