×

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba Amtembelea John Malecela Dodoma

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akiwa ameambatana na Mwenza wake Bi. Neema Nchemba, wamemtembelea na kumjulia hali Waziri Mkuu Mkuu mstaafu, John Malecela nyumbani kwake jijini Dodoma leo tarehe 18 Juni, 2026.

Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, akiwa ameambatana na mkewe, Bi. Neema Nchemba, wamemtembelea Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela, nyumbani kwake jijini Dodoma leo Juni 18, 2026.

Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kumjulia hali kiongozi huyo mkongwe wa Tanzania ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za juu serikalini na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa.

Hatua hiyo imeonyesha heshima na kuthamini mchango wa viongozi wastaafu katika ujenzi wa taifa, huku ikidhihirisha utamaduni wa viongozi wa sasa kuendelea kuwa karibu na waliowatangulia katika nafasi za uongozi.

Leave a Comment