×

Mabaunsa Wavamia Nyumba Ya Mjane Wa Mchungaji Mtikila, Kisa Mkopo Wa Milioni 250 Aliomdhamini Mtu – Video

Nyumba ya mjane wa marehemu Mchungaji Christopher Mtikila, Bi. Georgia Christopher Mtikila, iliyopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam, imekumbwa na taharuki baada ya watu wanaodaiwa kufika nyumbani kwake kutoa baadhi ya mali zake nje na kisha kubadilisha vitasa vya milango wakidai kuwa nyumba hiyo imeuzwa na benki.

Akizungumza na Global TV, Bi. Georgia amesema kuwa mwaka 2018 aliwahi kumdhamini kijana aitwaye Ramadhani Seif kupata mkopo wa benki wa shilingi milioni 250. Kwa mujibu wake, kijana huyo aliletwa kwake na rafiki wa marehemu mchungaji huyo kwa ajili ya kupata udhamini huo.

Bi. Georgia amesema kuwa Ramadhani Seif aliwahi kuanza kurejesha mkopo huo, lakini baadaye alishindwa kuendelea kufanya hivyo baada ya biashara yake kudorora na hatimaye kufeli.

Hata hivyo, hali hiyo imeibua sintofahamu kufuatia hatua ya watu hao kufika nyumbani kwake na kudai kuwa nyumba hiyo imeuzwa na benki kutokana na deni la mkopo huo.

Juhudi za kumpata Mwenyekiti wa Mtaa husika, Nelson Saidi, zinaendelea ili aweze kuzungumzia sakata hilo na kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu tukio hilo.

Leave a Comment