×

Fahamu Jinsi Lionel Messi Anavyoingiza Mabilioni Mbali na Mpira

Nyota wa soka duniani, Lionel Messi, ameendelea kuthibitisha kuwa mafanikio ya kweli hayaishii uwanjani pekee, bali hujengwa kupitia uwekezaji wa muda mrefu unaoweza kuendelea kuingiza mapato hata baada ya kustaafu kucheza.

Mbali na mafanikio yake makubwa ndani ya uwanja wa mpira, Messi amejenga himaya kubwa ya biashara inayojumuisha hoteli za kifahari nchini Spain, pamoja na uwekezaji katika sekta ya ukarimu na utalii nchini Andorra.

Uwekezaji huo unaonyesha mkakati wake wa kuangalia maisha baada ya soka kwa kumiliki mali na biashara zinazoweza kuzalisha thamani na mapato kwa miaka mingi ijayo.

Kwa wanamichezo wengi wakubwa duniani, utajiri wa kudumu haujengwi tu kupitia mishahara mikubwa na mikataba ya matangazo, bali kupitia umiliki wa biashara, mali na miradi inayoweza kuendelea kufanya kazi hata wanapostaafu.

Safari ya Messi ni mfano wa jinsi umaarufu unaotokana na mchezo unaweza kuwa daraja la kujenga himaya ya biashara na urithi wa kifedha wa muda mrefu.

Kama ambavyo wengi wanavyosema, mchezo huleta umaarufu, lakini umiliki wa mali na biashara ndio hujenga urithi wa kudumu.

Leave a Comment