
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Twaha Juma Lulengelule na kumteua kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Tabora.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Tanzania leo Juni 29, 2026, ACP Lulengelule alikuwa akihudumu kama Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) Mkoa wa Tabora kabla ya uhamisho huo.
Jeshi la Polisi limesema uteuzi huo umefanyika kuziba nafasi iliyoachwa wazi baada ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard George Abwao, kufariki dunia Juni 20, 2026.