Global TV inakaribisha maombi ya kazi kwa nafasi ya Motion Graphics Editor mwenye ubunifu na uwezo wa kuzalisha maudhui ya kisasa ya video kwa majukwaa ya kidijitali.
Nafasi hii inalenga kupata mtaalamu atakayesaidia kuimarisha ubora wa maudhui ya video kupitia ubunifu wa motion graphics unaoendana na viwango vya sasa vya utangazaji wa kidijitali.
Sifa za Mwombaji
- Awe na uzoefu wa kazi ya motion graphics na uhariri wa video (portfolio ni muhimu)
- Awe na ujuzi wa kutumia programu kama:
- Adobe After Effects
- Adobe Premiere Pro
- Adobe Photoshop
- Illustrator (ni faida ya ziada)
- Awe na uelewa wa kanuni za uhuishaji (animation principles) kama timing, keyframes, transitions na typography animation
- Awe na uwezo wa kutengeneza maudhui ya kuvutia kwa majukwaa ya kidijitali (YouTube, TikTok, Instagram, Facebook)
- Awe na uwezo mzuri wa kusimulia hadithi kupitia video (visual storytelling)
- Awe mbunifu, makini na mwenye macho ya kuona ubora wa kazi
- Awe na uwezo wa kufanya kazi kwa presha na kufuata muda wa mwisho wa kazi (deadlines)
- Awe tayari kufanya kazi kwa ushirikiano ndani ya timu na kupokea maoni ya kuboresha kazi
- Awe na uelewa wa msingi wa video formats na jinsi ya ku-export video kwa matumizi ya mitandao ya kijamii
- Ni faida ya ziada kama ana ujuzi wa sound design, 3D motion graphics au matumizi ya AI tools za video
Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji wanatakiwa kutuma CV na maelezo yao kupitia:
📧 [email protected]
☎️ +255 799 444 036
📍 Global Group House, Mori Road, Dar es Salaam
🗓 Mwisho wa kutuma maombi: 07 Julai 2026

