×

Manchester City Wavunja Benki Kumsajili Nyota Elliot Anderson

Klabu ya Manchester City imekamilisha usajili wa kiungo kijana Elliot Anderson kutoka Nottingham Forest kwa dau la rekodi ya pauni milioni 116 (TZS 371.2 bilioni), hatua inayomfanya kuwa mchezaji ghali zaidi wa Uingereza kuwahi kuuzwa.

Anderson, mwenye umri wa miaka 23, ameweka historia mpya kwa kupita rekodi ya awali iliyokuwa imewekwa na Jude Bellingham, ambaye usajili wake kwenda Real Madrid mwaka 2023 uligharimu takribani pauni milioni 115 (TZS 368 bilioni).

Nyota huyo ambaye kwa sasa yuko katika kikosi cha England kwenye Kombe la Dunia, anatajwa kuwa miongoni mwa viungo bora zaidi barani Ulaya kutokana na uwezo wake wa kudhibiti mchezo, kupiga pasi za mwisho na kusaidia mashambulizi.

Manchester City wameendelea kuimarisha kikosi chao kwa kusajili vipaji vya juu, huku usajili wa Anderson ukitarajiwa kuongeza nguvu zaidi kwenye safu yao ya kiungo kuelekea msimu ujao.

Hatua hiyo inaonyesha dhamira ya City kuendelea kubaki miongoni mwa vigogo wa soka la Ulaya kwa kuwekeza katika wachezaji vijana wenye uwezo mkubwa wa muda mrefu.

Leave a Comment