×

Nafasi za Customer Care Zatangazwa Dar, Mshahara wa Hadi Sh450,000

Wakazi wa Dar es Salaam, hususan wanawake wanaotafuta ajira, wamepata fursa mpya baada ya kutangazwa kwa nafasi za kazi za Customer Care katika Restaurant Posta na Maduka Mikocheni Plaza.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, waombaji watakaofanikiwa watapokea mshahara wa kati ya Sh400,000 hadi Sh450,000 kwa mwezi.

Waombaji wanatakiwa kuwa wanawake wanaoishi Dar es Salaam na wenye ujuzi wa kutoa huduma bora kwa wateja. Aidha, wanapaswa kuwa nadhifu, waaminifu na wenye maadili mazuri ya kazi.

Maombi yanapaswa kutumwa kupitia WhatsApp kwa namba 0703 854 777.

Mwisho wa kutuma maombi ni Julai 27, 2026.

Waombaji wote wenye sifa zinazohitajika wanashauriwa kutuma maombi yao mapema kabla ya tarehe ya mwisho ili kuongeza nafasi ya kuzingatiwa katika mchakato wa ajira.

Leave a Comment