
Msanii Billnass Julai 8, 2026 ameachia rasmi video ya wimbo wake “Hallo”, aliomshirikisha Nandy, ikiwa imeongozwa na Director Kenny.
Video hiyo imekuja na ubunifu wa hali ya juu, taswira za kuvutia na maandalizi yanayoifanya kuwa miongoni mwa video bora zilizotoka mwaka huu. Ikiwa ni kiashiria cha kile kinachokuja, mashabiki wa muziki wana kila sababu ya kutarajia ushindani mkubwa wa video za kiwango cha juu katika tasnia ya muziki mwaka huu.
Je, tayari umeitazama “Hallo”? Tuambie maoni yako kuhusu video hiyo kwenye sehemu ya maoni.