×

Wolper Afunguka Kuhusu Maisha ya Mastaa “Watu Huona Raha Tu, Hawajui Tunachopitia” – Video

Staa wa filamu za Bongo na mfanyabiashara maarufu, Jacqueline Wolper, amesema watu wengi huvutiwa na maisha wanayoishi mastaa bila kufahamu changamoto na misukosuko wanayopitia nyuma ya pazia.

Wolper ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, wakati alipokuwa pamoja na mastaa wenzake wanaounda kundi la A List, akiwemo Kajala Masanja, Irene Uwoya na Aunt Ezekiel.

Kwa mujibu wa Wolper, maisha ya umaarufu yanaonekana kuwa na furaha na mafanikio kwa nje, lakini ndani yake kuna mambo mengi ambayo mashabiki huwa hawayaoni.

Mkutano huo wa mastaa hao uliibua gumzo huku mashabiki wakisubiri kufahamu zaidi kuhusu jambo lililowakutanisha pamoja katika tukio hilo.

Leave a Comment