×

Fedha Zatawala Send Off ya Monalisa Buyamba, Zawadi Zimefikia Bilioni 1+ (Picha +Video)

Usiku wa kuamkia leo Jumatatu Julai 13, 2026 ulikuwa wa aina yake kwa familia ya Buyamba mkoani Geita baada ya kufanyika kwa send off ya Monalisa Buyamba, mtoto wa mfanyabiashara maarufu Mr. Buyamba, iliyohudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo watu wenye majina makubwa.

Katika hafla hiyo ya kifahari, Monalisa alipewa zawadi kubwa ya fedha inayotajwa kufikia Shilingi bilioni 1.004, huku wageni wengine wakiendelea kumwaga zawadi za fedha ukumbini.

Burudani ya usiku huo ilipamba moto zaidi baada ya msanii Alikiba kupanda jukwaani kutoa burudani kwa wageni. Wakati akiendelea kutumbuiza, msanii huyo alijikuta akipokea kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa wahudhuriaji, akiwemo baba wa Monalisa, ambao walimzawadia kutokana na kazi yake ya kuwaburudisha.

Hafla hiyo imeendelea kuwa gumzo mitandaoni kutokana na maandalizi yake ya kiwango cha juu, uwepo wa mastaa pamoja na aina ya zawadi zilizotolewa kwa binti huyo anayetarajiwa kuingia kwenye hatua mpya ya maisha.

Leave a Comment