×

Sendoff ya Kifahari: Mtoto wa GSM wa Katoro Aenda Kukagua Ukumbi kwa Chopa – Video

Maandalizi ya sendoff ya Monalisa Sylvester, mtoto wa mchimba madini maarufu wa Katoro, Geita, Sylvester Muyamba maarufu kama GSM wa Katoro, yameanza kuvuta hisia baada ya kuonekana yakifanyika kwa kiwango cha juu cha kifahari.

Katika picha zilizosambaa mitandaoni, Monalisa ambaye ni bi harusi mtarajiwa ameonekana akichukuliwa kwa chopa kutoka nyumbani kwao kijijini kwenda kukagua ukumbi wa tukio la sendoff yake.

 

Tukio hilo limezua gumzo kutokana na aina ya maandalizi yaliyoandaliwa, huku wengi wakishangazwa na matumizi ya chopa katika safari hiyo maalum ya kuelekea ukumbi wa sherehe.

Mandhari ya nyumbani kwao pamoja na maandalizi ya tukio hilo yameonyesha ukubwa wa hafla hiyo, huku mashabiki na watumiaji wa mitandao wakieleza kuvutiwa na namna familia hiyo inavyoweka mazingira ya kipekee kwa ajili ya siku hiyo muhimu.

Monalisa Sylvester ni mtoto wa mfanyabiashara na mchimba madini maarufu wa Katoro, Geita, Sylvester Muyamba, anayefahamika kwa jina la GSM wa Katoro.

Leave a Comment