
Kupitia Mradi wa Kuboresha Mfumo wa Usambazaji Maji katika Mji wa Misungwi, MWAUWASA imeendelea kuboresha upatikanaji wa huduma ya Maji safi na salama kwa wananchi.
Mradi huo, wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 880, umefikia asilimia 98 ya utekelezaji, huku zaidi ya wakazi 22,000 tayari wakianza kunufaika na maboresho yaliyotekelezwa.

Kukamilika kwa mradi huo kutainua kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji katika Mji wa Misungwi hadi asilimia 97, hatua itakayochangia kuboresha maisha ya wananchi pamoja na kuchochea maendeleo ya kiuchumi ya eneo hilo.
