
Msanii wa Bongo Fleva Marioo ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kushiriki picha kupitia ukurasa wake wa Instagram zinazoonekana kuashiria kuwa kuna tukio la ndoa lililofanyika.
Akiambatanisha picha hizo, Marioo aliandika ujumbe mfupi wa kumshukuru Mungu sambamba na kuwatakia Waislamu Ijumaa njema.
“Alhamdulillah 🙏 Jumaa Kareem,” aliandika Marioo.
Kilichoongeza gumzo ni maoni yaliyojitokeza chini ya chapisho hilo, ambapo Paula Kajala alimuita Marioo “mume wangu”, huku mashabiki wengi wakimpongeza msanii huyo na kutoa salamu za heri, jambo lililozua maswali iwapo wawili hao wamefunga ndoa kwa siri.

Wakati huohuo, Paula naye alichapisha picha kupitia ukurasa wake wa Instagram akisherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa Cape Town, Afrika Kusini.
Katika ujumbe wake aliandika:
Moyo wangu umejaa furaha. Asanteni sana kwa kila mmoja aliyepata muda wa kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa na kunitumia salamu za heri. Upendo wenu, dua zenu na maneno yenu ya kutia moyo vina maana kubwa sana kwangu. Ninashukuru sana. Nawapenda sana.
Miaka 24 nikiwa Cape Town.
Chapisho hilo limezidi kuchochea hisia za mashabiki, huku baadhi wakihusisha kauli ya “Birthday gift” na picha alizoshiriki Marioo.
Hata hivyo, hadi sasa Marioo na Paula hawajathibitisha rasmi kama wamefunga ndoa, hivyo kinachoendelea kubaki ni mjadala na hisia za mashabiki mitandaoni.
Je, unadhani Marioo na Paula wamefunga ndoa kimya kimya, au ni sehemu ya kiki za mastaa?
