×

MiXX Yakabidhi Zawadi kwa Washindi wa Kampeni ya Kombe la Dunia

Kampuni ya MiXX imeendelea kuwafurahisha wateja wake kupitia kampeni ya “Kombe la Dunia ya Ikiingia Tu… Golii!”, inayowapa nafasi watumiaji wa MiXX Super App kujishindia zawadi mbalimbali kwa kufanya malipo ya huduma kupitia programu hiyo.

Katika wiki ya nane ya kampeni hiyo, washindi sita walitangazwa, ambapo washindi wanne walijinyakulia zawadi ya fedha taslimu ya Shilingi milioni moja kila mmoja, huku washindi wawili wakiondoka na vifaa vya kisasa vya kampuni ya Hisense.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Malipo ya Kidijitali wa MiXX, Mshamma Mshamma, alisema kampeni hiyo imeendelea kupata mwitikio mkubwa kutoka kwa Watanzania, huku jumla ya washindi 80 wakiwa tayari wamenufaika tangu ilipoanza.

Mshamma alisema washindi wamekuwa wakipata nafasi ya kujishindia fedha taslimu pamoja na vifaa mbalimbali kupitia ushirikiano wao na kampuni ya Hisense, hatua inayoonyesha dhamira ya MiXX kuwathamini na kuwazawadia wateja wake waaminifu.

Alibainisha kuwa kampeni hiyo bado inaendelea, huku akieleza kuwa mshindi wa mwisho wa kampeni hiyo ataondoka na zawadi kubwa ya Shilingi milioni 50.

Aliwahimiza wananchi kuendelea kutumia MiXX Super App kufanya malipo mbalimbali ya huduma za kifedha ili kuongeza nafasi zao za kushinda zawadi hizo.

“MiXX Super App ni zaidi ya programu ya malipo. Ni jukwaa linalorahisisha huduma za kifedha huku likiwapa watumiaji nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali,” alisema Mshamma.

Mmoja wa washindi, Ibrahim Mandoa, mkazi wa Kinondoni, alisema ushindi huo umempa imani kuwa kampeni hiyo ni ya kweli na inaleta manufaa kwa watumiaji wa MiXX Super App.

“Nimefurahi sana kushinda na hii ni mara yangu ya kwanza kupata zawadi kama hii. Nawahimiza Watanzania kuipakua na kuitumia MiXX Super App mara kwa mara kufanya malipo mbalimbali ili nao wapate nafasi ya kushinda,” alisema Mandoa.

Kampeni ya “Kombe la Dunia ya Ikiingia Tu… Golii!” inaendelea kutoa nafasi kwa watumiaji wa MiXX Super App kushinda zawadi mbalimbali hadi kufikia zawadi kuu ya Sh milioni 50.

Leave a Comment