×

Rais Samia Azindua Ujenzi wa Meli Nne za Mizigo Bandari ya Kigoma (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Plasduce Mbossa akitoa maelezo kuhusu ujenzi na ukarabati wa meli kabla ya uzinduzi uliofanyika katika bandari ya Kigoma mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Julai 20, 2026, amezindua rasmi mradi wa ujenzi wa meli nne za mizigo katika Bandari ya Kigoma, hatua inayolenga kuimarisha usafirishaji wa mizigo katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika.

Uzinduzi huo umefanyika wakati wa ziara ya Rais Samia mkoani Kigoma, ambapo amesema mradi huo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuboresha miundombinu ya uchukuzi na kuongeza ufanisi wa huduma za bandari ili kuchochea biashara na ukuaji wa uchumi.

Rais Samia akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Meli 4 za mizigo zitakazo hudumu katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma, tarehe 20 Julai

Meli hizo zinatarajiwa kuongeza uwezo wa kusafirisha mizigo ndani na nje ya Tanzania kupitia Ziwa Tanganyika, huku zikirahisisha shughuli za kibiashara kati ya Tanzania na nchi jirani zinazotumia ziwa hilo, ikiwemo Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Zambia.

Mradi huo unasimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na unatarajiwa kuimarisha nafasi ya Bandari ya Kigoma kama kitovu muhimu cha usafirishaji na biashara katika ukanda wa Maziwa Makuu.

Rais Samia akipiga kengele kuashiria uzinduzi wa Meli 4 za mizigo.
Matukio mbalimbali katika uzinduzi wa Meli 4 za mizigo zitakazo hudumu katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma, tarehe 20 Julai, 2026.

Leave a Comment