
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetangaza nafasi 44 za kazi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za Wakufunzi Wasaidizi Maendeleo ya Jamii II katika fani mbalimbali.
Nafasi hizo zinahusisha ufundi na taaluma mbalimbali kama ifuatavyo:
- Mkufunzi Msaidizi Maendeleo ya Jamii II – Ushonaji na Ubunifu wa Mitindo (Tailoring and Fashion Design) – Nafasi 10
- Mkufunzi Msaidizi Maendeleo ya Jamii II – Uchomeleaji na Utengenezaji wa Vyuma (Welding and Metal Fabrication) – Nafasi 13
- Mkufunzi Msaidizi Maendeleo ya Jamii II – Uandaaji wa Chakula (Food Production) – Nafasi 2
- Mkufunzi Msaidizi Maendeleo ya Jamii II – Magari (Motor Vehicle Mechanics) – Nafasi 5
- Mkufunzi Msaidizi Maendeleo ya Jamii II – Useremala (Carpentry and Joinery) – Nafasi 9
- Mkufunzi Msaidizi Maendeleo ya Jamii II – Uhazili (Secretarial Studies) – Nafasi 5
Waombaji wanatakiwa kuwa wamehitimu Kidato cha Nne au Sita na kuwa na Stashahada (Diploma) katika fani husika kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Majukumu ya Wakufunzi
Watakaopata nafasi watahusika na majukumu mbalimbali ikiwemo:
- Kufundisha masomo ya fani zinazotolewa chuoni;
- Kuandaa mipango ya kazi za mafunzo;
- Kupima maendeleo ya wanachuo katika nadharia na vitendo;
- Kutunza vifaa vya kufundishia;
- Kufanya tafiti na kutoa taarifa;
- Kutoa ushauri wa kitaalam;
- Kutunga na kusahihisha mitihani;
- Kuandaa taratibu za kusimamia mitihani;
- Kuboresha taaluma chuoni na kuendeleza programu za mafunzo nje ya chuo.
Mshahara
Nafasi zote zipo katika ngazi ya mshahara TGS C.
Masharti ya Waombaji
Waombaji wanapaswa:
- Kuwa raia wa Tanzania;
- Kutokuwa na umri zaidi ya miaka 45;
- Kuwasilisha cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili;
- Kuambatanisha vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa;
- Kutuma maombi kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 31 Julai 2026.
Maombi yawasilishwe kupitia Recruitment Portal ya Sekretarieti ya Ajira:
Waombaji wanakumbushwa kuwa mchakato wa ajira unazingatia haki, usawa na uwazi, huku vitendo vya rushwa vikikatazwa.
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WIZARA YA ELIMU 18-07-2026