
Klabu ya Yanga imeendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya baada ya kutangaza rasmi usajili wa wachezaji wawili kutoka Mashujaa FC ya Kigoma.
Yanga imemaliza usajili wa mshambuliaji Hussein Mihambo, ambaye anajiunga na mabingwa hao wa Tanzania Bara kwa lengo la kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji kufuatia kuondoka kwa mshambuliaji Prince Mpumelelo Dube.
Sambamba na hilo, klabu hiyo imemtambulisha pia beki wa kulia Abdulnassir Assa ‘Gamal’, aliyesaini mkataba wa miaka miwili akitokea Mashujaa FC.

Mbali na kucheza nafasi ya beki wa kulia, Gamal pia ana uwezo wa kucheza kama winga wa kulia anayepanda na kushuka, jambo linalompa kocha chaguo zaidi kutokana na ubora wake wa kucheza katika nafasi tofauti.
Usajili wa Mihambo na Gamal unaonyesha dhamira ya Yanga ya kuendelea kukisuka kikosi chenye ushindani mkubwa kwa ajili ya michuano ya ndani na kimataifa katika msimu wa 2026/27.