×

Aliyekuwa Kocha wa Makipa wa Simba na Wenzake Wafikishwa Tena Kisutu

Aliyekuwa kocha wa makipa wa Klabu ya Simba, Muharami Sultani, pamoja na wenzake, wamefikishwa tena leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kwa ajili ya kuendelea na kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Sultani na wenzake wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 71/2022, inayohusisha jumla ya mashtaka manane, yakiwemo ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroini zenye uzito wa kilo 34.89.

Washtakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 21, 2022. Baadaye kesi hiyo ilihamishiwa Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, ambako ilianza kusikilizwa huku washtakiwa wote wakikana mashtaka yanayowakabili.

Baada ya hatua mbalimbali za kisheria, washtakiwa waliachiwa, lakini muda mfupi baadaye walikamatwa tena nakufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kuendelea na mchakato wa kesi yao.

Leave a Comment