
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameungana na familia, waumini, viongozi mbalimbali pamoja na wananchi katika Misa Takatifu ya kumbukumbu ya miaka sita tangu kufariki kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa.

Ibada hiyo ilifanyika leo, Julai 23, 2026, katika Kanisa Katoliki la Parokia ya Mtakatifu Immaculate, Upanga, jijini Dar es Salaam, ambapo washiriki walipata nafasi ya kumuenzi na kumkumbuka Hayati Mkapa kwa mchango wake mkubwa katika uongozi na maendeleo ya Tanzania.
Misa hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa Serikali, viongozi wa dini, ndugu wa familia ya Hayati Mkapa pamoja na waumini na wananchi waliofika kutoa heshima zao kwa mmoja wa viongozi waliowahi kuliongoza taifa.

