×

Rais Dkt. Mwinyi Awaapisha Viongozi Wanne, Wakiwemo Majaji Wawili wa Mahakama Kuu Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo Julai 24, 2026, amewaapisha viongozi wanne aliowateua hivi karibuni, wakiwemo majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Hafla ya kuapishwa imefanyika Ikulu, Zanzibar, ambapo viongozi hao wamekula kiapo cha uadilifu na kuanza rasmi kutekeleza majukumu yao.

Walioapishwa ni Dkt. Mahadhi Juma Maalim, aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar; Mhe. Valentina Andrew Katema, Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar; Mhe. Khamis Ali Simai, Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar; pamoja na Dkt. Josephine Rogate Kimaro, aliyeteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla; Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla; Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mhe. Zuberi Ali Maulid; Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Ndg. Mansoura Mossi Kassim; Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, viongozi wa dini pamoja na wageni wengine waalikwa.

Leave a Comment