×

Washindi Zaidi ya 90 Wanufaika Kampeni ya Mixx “Ikiingia Tu Goli”

Dar es Salaam, Julai 24, 2026 – Kampuni ya huduma za fedha kidijitali Mixx imewataka Watanzania kuendelea kutumia huduma zake huku ikitangaza kuwa mshindi wa mwisho wa kampeni ya “Ikiingia Tu Goli” anatarajiwa kujishindia zawadi ya Shilingi milioni 50 wiki ijayo.

Kampeni hiyo inayofanyika kwa ushirikiano na Hisense imeendelea kuwapa Watanzania fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali, ambapo hadi sasa zaidi ya watu 90 wamenufaika tangu kuanza kwa promosheni hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya tisa ya kampeni hiyo, Mkuu wa Idara ya Makampuni na Washirika wa Mixx, Bw. Justine Lawena, alisema kampeni hiyo imelenga kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali huku ikiendelea kuwazawadia watumiaji.

Katika droo hiyo, washindi 10 walipatikana, ambapo washindi saba walijishindia Shilingi milioni moja kila mmoja, huku watatu wakipata vifaa vya kampuni ya Hisense.

Lawena alisema licha ya fainali za Kombe la Dunia kumalizika, sasa kinachofuata ni fainali ya kampeni hiyo ambayo itatoa zawadi kubwa zaidi ya Shilingi milioni 50 kwa mshindi mmoja.

“Fainali za Kombe la Dunia zimekwisha, lakini fainali ya kampeni yetu ndiyo inafuata wiki ijayo. Hapo ndipo tutampata mshindi wa Shilingi milioni 50. Bado kila Mtanzania ana nafasi ya kushinda kwa kutumia Mixx Super App,” alisema.

Alieleza kuwa ili kushiriki droo ya mwisho, wateja wanatakiwa kutumia Mixx Super App kufanya miamala mbalimbali ikiwemo kutuma na kupokea fedha, kulipa bili pamoja na kufanya malipo ya Serikali.

Aidha, aliwataka wateja kuwa makini wanapopokea simu za taarifa za ushindi, akisisitiza kuwa namba rasmi ya Mixx kwa ajili ya kuwajulisha washindi ni 100.

“Tunawakumbusha wateja kupokea simu kutoka namba 100. Usipoipokea unaweza kupoteza fursa ya kuthibitisha ushindi wako. Bado una nafasi ya kushinda kwa kuendelea kutumia Mixx Super App,” alisema Lawena.

Mmoja wa washindi wa Shilingi milioni moja, David Kisusi, alisema ushindi huo umempa hamasa zaidi ya kuendelea kutumia huduma za Mixx kutokana na urahisi na usalama wake.

Alisema amekuwa akitumia Mixx kwa shughuli zake za kila siku, ikiwemo kulipia bili mbalimbali kupitia simu yake, huku akivutiwa zaidi na mfumo wa usalama wa huduma hizo.

Kampeni ya “Ikiingia Tu Goli” kati ya Mixx na Hisense inaendelea kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali nchini, huku Watanzania wakisubiri kutajwa kwa mshindi wa zawadi kuu ya Shilingi milioni 50.

Leave a Comment