×

Ikulu Tunguu: Rais Samia Awaapisha Viongozi Wapya wa Serikali

Rais Dkt. Samia akimuapisha Dkt. Latifa Mohammed Khamis kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Tunguu Zanzibar, tarehe 27 Julai, 2026.

Zanzibar – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Julai 27, 2026, amewaapisha viongozi wawili kushika nafasi za Naibu Katibu Mkuu katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Tunguu, Zanzibar.

Katika hafla hiyo, Rais Samia amemuapisha Dkt. Latifa Mohammed Khamis kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano.

Aidha, amemuapisha Ndugu Prisca Burton Lwangili kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Rais Samia akimuapisha Ndugu Prisca Burton Lwangili kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Tunguu Zanzibar, tarehe 27 Julai, 2026.

Viongozi Wateule wakiapa kiapo cha uadilifu kwa Viongozi wa Umma kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Tunguu Zanzibar, tarehe 27 Julai, 2026.

 

Leave a Comment