
Zinedine Zidane ameteuliwa rasmi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa akichukua nafasi ya Didier Deschamps ambaye ameondoka baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka 14.
Deschamps alihitimisha kipindi chake cha uongozi kufuatia Ufaransa kutolewa katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia la 2026 baada ya kufungwa na Spain national football team.
Zidane, ambaye aliisaidia Ufaransa kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1998 akiwa mchezaji, amekuwa nje ya ukocha tangu alipoondoka Real Madrid CF mwaka 2021 baada ya kipindi chake cha pili kuinoa klabu hiyo.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 54 amesaini mkataba utakaomuweka madarakani hadi kipindi cha kufuzu Kombe la Dunia la 2030.
Akizungumza baada ya uteuzi huo, Zidane alisema ni heshima kubwa kupewa nafasi ya kuiongoza timu ya taifa ya nchi yake.

“Hakuna kitu kikubwa zaidi kuliko timu ya taifa ya Ufaransa. Ni furaha na fahari kubwa kuwa kocha wa Les Bleus,” alisema Zidane.
Rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa, Philippe Diallo, alimwelezea Zidane kama nguli wa soka la Ufaransa na mmoja wa makocha waliofanikiwa zaidi duniani.
Mechi ya kwanza ya ushindani ya Zidane akiwa kocha wa Ufaransa itakuwa dhidi ya Uturuki katika michuano ya UEFA, Septemba 25, 2026.